Tuesday, January 17, 2012

Facebook yamponza Flora Mbasha

Facebook yamponza Flora Mbasha

Mwanamuziki maarufu wa injili Florah Mbasha
MTANDAO maarufu wa kijamii wa Facebook umemponza msanii mahiri wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Flora Mbasha, baada ya mtu asiyefahamika ambaye ni shabiki wake kugandisha picha chafu za ngono kwenye ukurasa wake ambayo iliibuka mijadala na kushangaza wengi wiki iliyopita.

Mbasha aliyetamba na nyimbo kama 'Adui', 'Usife Moyo', 'Sauti ya Mnyonge' aliibuka kwenye mtandao huo na kutoa ufafanuzi.

"Bwana Yesu asifiwe wapendwa, naomba niwatake radhi kwa picha ambayo ilikuwa imetupiwa kwenye ukurasa wangu pia niwashukuru wote ambao mmenipigia simu kunieleza kinachoendelea kwenye Facebook yangu, pia nawashukuru wote mlionielekeza jinsi ya kuifuta maana nilijaribu nikashindwa.

"Lakini pia nimuombe anayetupia picha kama hizi kwenye ukurasa wangu aache upesi la sivyo nitaifunga mtu yeyote asitupie vitu vyake ingawa haikuwa nia yangu kwani hii ni kwa ajili ya Injili, watumishi wa Mungu kukutana kuzungumzia habari za Mungu na marafiki mbalimbali kuelimishana kuhusu Injili na mambo yote yenye maadili na sio jambo lisilompendeza Mungu.

"Kwa upande wangu nimekwazika sana kwani sikutegemea kama mtu mwenye akili timamu angefanya hivyo, ila nimemsamehe. Nia yangu ni nzuri sana, nataka watu tujadili mambo ya Mungu, tushauriane na hasa kutokana na huduma ya uimbaji niliyo nayo nahitaji sana ushauri wenu na mawazo.

"Pia niwashirikishe mambo mbalimbali kuhusu maisha yangu binafsi pamoja na huduma, ili kwa pamoja tuonyane na tusaidiane pamoja na kuombeana. Nawapenda sana wote na amani ya Yesu Kristo iwe nanyi."  CHANZO..GAZETI LA MWANASPOTI LA LEO 17 January 2012
      

No comments:

Post a Comment